24 Oktoba 2025 - 20:55
Mratibu JMAT-TAIFA | Na Balozi wa Amani Dunia - Bi.Fatma Kikkides, atoa wito wa Kitaifa wa Kulinda Amani:  “Amani ni jukumu la vijana wote”

"Vijana ndio nguzo kuu ya Taifa na nguvu kazi inayotegemewa. Ni jukumu lenu kulinda amani tuliyonayo na kuhakikisha vizazi vijavyo vinairithi. Amani inaanzia kwenye nafsi, nyumbani na hata sehemu za kazi,” alisema Bi. Kikkides.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (AS) -ABNA-Mratibu wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT-TAIFA), ambaye pia ni Balozi wa Amani wa Taasisi ya Wanawake nchini Korea Kusini, Bi. Fatma Fredrick Kikkides, ametoa wito maalum kwa vijana nchini kuhakikisha wanalinda amani iliyopo na kuepuka kudanganyika na ushawishi wa mitandao ya kijamii.

Mratibu wa JMAT-TAIFA | Na Balozi wa Amani Dunia - Bi.Fatma Kikkides, atoa wito wa Kitaifa wa Kulinda Amani:  “Amani ni jukumu la vijana wote”

Akizungumza katika mahojiano maalum na Televisheni ya Taifa (TBC2) tarehe 23 Oktoba 2024, Bi. Kikkides alisisitiza umuhimu wa vijana kutambua nafasi yao katika ujenzi wa Taifa na katika kuendeleza amani ya kudumu.

“Vijana ndio nguzo kuu ya Taifa na nguvu kazi inayotegemewa. Ni jukumu lenu kulinda amani tuliyonayo na kuhakikisha vizazi vijavyo vinairithi. Amani inaanzia kwenye nafsi, nyumbani na hata sehemu za kazi,” alisema Bi. Kikkides.

Mratibu wa JMAT-TAIFA | Na Balozi wa Amani Dunia - Bi.Fatma Kikkides, atoa wito wa Kitaifa wa Kulinda Amani:  “Amani ni jukumu la vijana wote”

Aidha, aliwahimiza vijana kutambua thamani ya amani na kujiepusha na makundi yenye misimamo mikali yanayotumia mitandao ya kijamii kueneza chuki, migawanyiko na taharuki nchini.

“Msikubali kushawishiwa na watu wasiokuwa na nia njema. Wapo wanaotumia mitandao kuharibu umoja wa Taifa, lakini ni wajibu wenu vijana kusimama imara na kuitetea nchi yenu,” aliongeza.

Bi. Kikkides alieleza kuwa moja ya changamoto kubwa kwa vijana ni ukosefu wa elimu ya amani na matumaini, hali inayowasukuma kujiunga na makundi hatarishi kwa sababu ya hasira na kukata tamaa kutokana na ukosefu wa ajira.

“Tunapaswa kuwajengea vijana uelewa juu ya thamani ya amani. Wengi wanapotea kwa kukosa matumaini, lakini ni lazima watambue kuwa amani ni urithi wa thamani mkubwa kuliko mali yoyote,” alisisitiza.

Mratibu wa JMAT-TAIFA | Na Balozi wa Amani Dunia - Bi.Fatma Kikkides, atoa wito wa Kitaifa wa Kulinda Amani:  “Amani ni jukumu la vijana wote”

Kwa ujumla, alitoa rai kwa taasisi za elimu, dini, na jamii kushirikiana katika kuimarisha elimu ya amani, akibainisha kuwa bila amani hakuna maendeleo endelevu yanayoweza kupatikana.

Your Comment

You are replying to: .
captcha